TAARIFA KWA DIASPORA NA UMMA WA WATANZANIA

TAARIFA KWA DIASPORA NA UMMA WA WATANZANIA

Baraza la Diaspora wa Tanzania Duniani – Tanzania Global Diaspora Council (TDC GLOBAL), linayo furaha kubwa kuutangazia umma wa Watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) na wale waishio nyumbani Tanzania kuwa limekamilisha usajili wake nchini Sweden tarehe 18 May 2018. TDC Global imesajiliwa kama taasisi ya hiari na isiyo ya kibiashara (Non Profit organisation). Namba yake ya Usajili ni 802516-6979 na anwani ya posta ni Box 1089, 10139 Stockholm, Sweden. Namba za simu kwa shughuli za kiofisi ni +46 729 165 552 na
+46 739 484 288. Barua Pepe ni: info@tdcglobal.org na tovuti ni: www.tdcglobal.org

Lengo kuu la baraza hili ni kuwaunganisha watanzania wote wanaoishi ughaibuni katika chombo kimoja TDC Global, kitakachokuwa mwakilishi wa mambo yote yanayohusu diaspora huko wanapoishi na nyumbani Tanzania. Halikadhalika, TDC Global ina lengo la kuunganisha nguvu za Diaspora ili kuchangia kukuza uchumi wa nchi yetu Tanzania na kuleta maendeleo chanya kwa Wananchi wote wa Tanzania waliopo nyumbani na nje ya nchi.

Pamoja na kutangaza usajili wetu, baraza linapenda pia kuwatambulisha kwa umma viongozi wake, Wajumbe wa kamati ya utendaji na wajumbe wa kamati ya uteuzi. Picha, Majina, nafasi zao za uongozi na namba zao za simu zinaonekana hapo chini .

Uongozi wa TDC Global unapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zake za dhati kwa viongozi wote wa Vyama vya Diaspora vilivyoshirikiana na viongozi wa baraza na waanzilishi wa TDC Global, kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi kufanikisha Tanzania Global Diaspora Council kuwa taasisi kamili. Mungu awabariki sana. Wote walifanya kazi hii kwa moyo sana na kwa kujitolea bila malipo. Tuna imani kuwa wataendelea kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kusaidia kufikia malengo ya baraza kwa pamoja na kwa haraka zaidi.

Tunarudia tena kuwashukuru wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika safari hii ndefu ya usajili wa TDC Global. Asanteni sana na mwenyezi Mungu awabariki.

Simu za Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji

01. Mwenyekiti. Simu +46 72 916 55 52
02. Makamu Mwenyekiti. Simu +35 84 5180 920
03. Katibu. Simu +46 739 484 288
04. Naibu Katibu. Simu +46 704 956 650
05. Katibu wa Hazina. Simu +46 706 508 823
06. Naibu Katibu wa Hazina. Simu +256 782 989 330
07. Mjumbe wa kamati ya utendaji (Bi. E. Pedersen) Simu +46 725 145 750
08. Mjumbe wa kamati ya utendaji (Bi. N. Kitilya) Simu +44 794 646 7394
09. Mjumbe wa kamati ya utendaji ( Bw. T. Kilumanga) Simu +46 705 263 303
10. Mjumbe wa kamati ya utendaji (Bi. F. Ndaro) Simu +1 316 350 4527
11. Mjumbe wa kamati ya utendaji (Bi. B. Razafinjatovo) +32 479 470 927
12. Mjumbe wa kamati ya utendaji (Bw. L. Mukami) +1 301 661 6696
13. Mjumbe wa kamati ya Uteuzi (Bw. J. Msangi) +1 6475 018 317
14. Mjumbe wa kamati ya Uteuzi (Bw. H. Nganzo) +47 472 62 181
15. Mjumbe wa kamati ya Uteuzi (Bw. J. Warioba) +44 7570 773 369
16. Mjumbe wa Kamati ya Uteuzi (Bi. B. Kyelu) +61451694804
17. Mjumbe wa Kamati ya Uteuzi (Bw. B. Kazora) +12698730937
18. Mjumbe wa Kamati ya Uteuzi (Dkt C.M Tungaraza) +61413772269

Share this post

Comments (2)

 • Hodari Mchemba
  Hodari Mchemba Reply

  Nawashukuru wote mliofikiria kuanzisha umoja huu Mungu awabariki sana.
  Nimefurahi kujiunga wala sikusumbuka hata chembe naahidi kuwatangazia wenzetu ambao huenda hawajuwi kama tumepata chombo cha kubeba na kutetea haki zetu sisi watanzania waishio ughaibuni na ndani ya Tanzania.

  AHSANTE
  Hodari Varberg Halland Region

  August 13, 2018 at 8:30 pm
 • Matthew Paulo Sanka
  Matthew Paulo Sanka Reply

  habari kwa ndugu zangu wote humu nami niwashukuru wale wote waliojitolea kuanzisha chombo hiki ili mawazo na hisia za wa-Tanzania waishio ughaibuni zipate nafasi na uwakilishi. Mungu awabariki sana. Mungu ibariki nchi yetu, Tanzania. asanteni.

  August 14, 2018 at 6:50 pm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


X