TDC Global

TDC Global

Diaspora Na Nyumbani 2021

Mwenyekiti wa TDC Global, Bi Bupe Amon Kyelu akitoa taarifa kuhusu tukio kubwa la TDC Global linalojulikana kwa jina la Diaspora Na Nyumbani 2021 Ambalo linatarajiwa kufanyika mjini Dodoma nchini Tanzania mwezi wa 6 2021.

Pamoja na masuala mengine, Mwenyekiti wa TD Global, amewataka watanzania wote waishio kwenye maeneo mbalimbali duniani, kujiunga na kuwa pamoja ili kuendelea nguvu ya upamoja ya kuwezesha chachu ya maendeleo nyumbani. 

Mwenyekiti ameelezea pia hatua kubwa ya ukusanyaji wa maoni ya mapendekezo ya Hadhi maalum kwa Diaspora ya Tanzania kwa serikali, na kwamba zoezi hilo lilifanyika na kufanikiwa kwa uzuri kabisa na kwamba matokeo ya mapendekezo hayo, yamesha kabidhiwa na kupokelewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Na yanafanyiwa kazi.

Mwenyekiti Bi Bupe Kyelu, ametoa mwito kwa wanajumuia wa diaspora ya kitanzania, kutenga muda na viwezeshi kwa ajili ya kuhudhuria na kuhusika kwenye tukio la kihistoria la Diaspora na Nyumbani 2021 ambalo linaweka alama kubwa ya watanzania walio katika maeneo mbalimbali nje ya nchi, kukutana Nyumbani kwa malengo ya kuijenga jumuia ya TDC, umoja, udugu na uzalendo kwa nchi yao Tanzania.

Taarifa zaidi kuhusu tukio la Diaspora na Nyumbani 2021 zitaendelea kuletwa kwenu kupitia tovuti hii na vyanzo vingine vya taarifa vya TDC Global.

Imetolewa na Uongozi TDC Global 
Dec 2020

 

Share this post