FOMU YA MSHIRIKI MTOA HUDUMA MKUTANO WA DIASPORA

TDC Global inawakaribisha Diaspora Watanzania kujisajili kutoa huduma za kijamii za kujitolea katika mkutano wa diaspora maarufu DIASPORA NA NYUMBANI 2021 utakaofanyika jijini Dodoma Tanzania kuanzia tarehe 23 hadi 26 June 2021.

Diaspora wote kupitia taaluma zao na ujuzi wanaweza kushiriki katika siku mbili za makambi za kutoa huduma, mwisho wa kujisajili ni tarehe 28 Februari 2021. Uongozi wa TDC Global utawapanga washiriki kutokana na idadi yao,taaluma na ujuzi ili kuwawezesha kutoa huduma tarajiwa. Huduma zinazotegemewa kutolewa ni:

  1. Huduma za Afya
  2. Huduma za Kijamii
  3. Huduma za mafunzo
  4. Huduma za Burudani, (Sanaa, Utamaduni na michezo)
  5. Huduma za mazingira
  6. Huduma nyinginezo (Tafadhari elezea zaidi hapo chini Maelezo ya ziada)

Kwa msaada wa haraka tuma barua pepe kwa: naibu.katibumkuu@tdcglobal.org au WhatsApp:+46704956650.
Uongozi wa TDC Global unatanguliza shukrani kwa ushiriki wako, upatapo taarifa hizi mjulishe Diaspora mwingine. Tukutane Dodoma.