MAELEZO MUHIMU SANA KWA WANAOHITAJI MWALIKO KWA AJILI YA VIZA

Home_backup Forums TDC LAUNCH APRIL 9-11-2019 MAELEZO MUHIMU SANA KWA WANAOHITAJI MWALIKO KWA AJILI YA VIZA

Viewing 1 post (of 1 total)
 • Author
  Posts
 • #3028
  mrina
  Keymaster
  @mrina

  TAFADHALI SOMA KWA MAKINI

  MAELEZO MUHIMU SANA KWA WANAOHITAJI MWALIKO KWA AJILI YA VIZA TU

  Kama wewe ni miongoni mwa watu/Diaspora watakaohitaji viza kuingia nchini Sweden kwa ajili ya Kongamano La Uwekezaji na uzinduzi rasmi wa Baraza La Diaspora Ya Watanzania Duniani(TDC Global),na utahitaji kupata mualiko kutoka TDC Global kwa ajili ya kuombea viza. TDC Global inakuomba ushirikiano wako ili kulifanikisha jambo hilo kwa haraka, TDC Global inakuomba kuwasilisha kwetu vitu vifuatavyo:

  1. Kivuli (copy) ya passport yako kwenye kurasa zinazoonyesha jina lako kamili, tarehe ya kuzaliwa, nambari ya pasi ya kusafiria (passport), nchi na mahali ilipotolewa na muda wa kuisha matumizi yake (expiration date)

  2. Tarehe unayotarajia kuingia na kutoka Sweden( tunapendekeza uandike japo siku 3 kabla ya Kongamano kuingia na siku 3 baada ya Kongamano ili kuepuka usumbufu wa kulazimika kuingia na kutoka kwa haraka katika siku za kongamano)

  3. Nchi ulipo ubalozi utakaoenda kuomba visa yako. Ikiwezekana na anwani ya ubalozi huo.
  Tuma taarifa hizo hapo juu kwa barua pepe yetu maalum ya viza@tdcglobal.org mapema iwezekanavyo. Tafadhali zingatia kwamba TDC Global itatoa mwaliko pindi tu utakapokuwa umekamilisha malipo ya malazi na chakula kwa siku zote za Kongamano na kuwakilisha taarifa zilizotajwa hapo juu (namba moja hadi tatu.)

  Kulipia malipo hayo ya malazi na chakula kwa siku za Kongamano bonyeza tovuti hii hapa https://www.tallinksilja.se/tdcglobal . Kwa Diaspora tu, Unashauriwa kujiunga pia uanachama wa TDC Global kupitia tovuti https://tdcglobal.org/iump-register/ . Hii itakusaidia pia katika maombi yako ya viza kwa kueleze kuwa unakuja pia kwenye mkutano mkuu kama mwanachama. kujiunga na TDC Global kwa sasa ni bure.
  Ukiwa na swali lolote la ziada unaweza kupiga au kutuma ujumbe kwa simu namba +4747262181 au +46739484288.
  NB. Tunakuomba usome vizuri maelezo yaliyopo hapo juu na kuyatekeleza kwanza kabla ya kutuma maswali kwenye namba hizo, Kufanya hivyo kutapunguza usumbufu kwa pande zote mbili.

  Mwisho tunapenda kukumbusha kwamba, TDC Global imeandaa Kongamano hili, kwa maana ya kwamba katika malipo yoyote utakayolipia hakuna pesa itakayokwenda kwa TDC Global.

  ’’ Pamoja Tunaweza, Mtu kwao Ndiyo Ngao’’

  Agnes Lerdorf
  Mwenyekiti wa Mahusiano ya Umma
  TDC Global – Denmark.
  2019-02-22

Viewing 1 post (of 1 total)
 • You must be logged in to reply to this topic.