Baraza la Diaspora Watanzania Dunian – TDC Global kwa heshima kubwa linawatangazia Diaspora Watanzania Duniani kuzinduliwa rasmi kwa usajili wa ushiriki wa mkutano mkuu na siku ya Diaspora Watanzania Duniani vitakavyo fanyika kuanzia tarehe 23 Juni 2021 mpaka 26 Juni 2021 mjini Dodoma Tanzania.
Kila mshiriki wa mkutano huo anatakiwa kujisajili na kulipa gharama za ushiriki na huduma zitakazo tolewa wakati wa mkutano huo kwa kupitia tovuti ifuatayo.
https://tdcglobal.org/diasporadodoma2021
TDC Global inawaomba Diaspora wote kujisajili mapema ili kusaidia kufanikisha maandalizi ya mkutano huo kwa pande zote, yaani TDC Global na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa anuani pepe info@tdcglobal.org
Diaspora na Nyumbani 2021.
Imetolewa na Uongozi TDC Global
Bi Bupe Amon Kyelu
Mwenyekiti
04 January 2021