TDC Global
TDC Global

TDC Global

Mabadiliko Ya Mkutano Mkuu TDC Global 2022

Baraza la Diaspora Watanzania Duniani -TDC Global linawatangazia Wanachama na Umma kuwa, Mkutano Mkuu na uchaguzi wa viongozi uliokuwa unatarajiwa kufanyika tarehe 21 hadi 23 Julai 2022 jijini Dodoma Tanzania umebadilishwa. Badala yake mkutano huo utafanyika tarehe 23 Julai 2022 kwa njia ya mtandao.

Taratibu za kushiriki Mkutano Mkuu na uchaguzi wa Viongozi wa TDC Global zitatolewa kwa kadri zinavyokamilika. Uongozi unawakumbusha wanachama kulia Ada zao, ili wakidhi vigezo vya kikatiba vya kuchagua na kuchaguliwa kupitia mkutano huo.

Mabadiliko ya mkutano huu yamesababishwa na kuingiliana na ratiba ya kongamano la Diaspora linalotarajiwa kufanyika nchini Tanzania, chini ya usimamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakao jitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

Kwa mawasiliano zaidi tafadhali tuandikie kupitia anuani pepe: maoni@tdcglobal.org

TDC Global inatoa shukrani za dhati kwa wanachama na umma kwa ushirikiano mnaotupatia.
Asanteni sana

“Diaspora na Nyumbani“

TANGAZO MKUTANO MKUU 2022 MTANDAONI

Share this post