1. Urahisi wakupata barua ya kukutambulisha Tanzania na kuweza kupata misaada na huduma za haraka kwani mda wako Tanzania ni mfupi.
  2. Kama una anzisha mradi na unapitia kwenye TDC G na TDC G chamber of Commerce utakuwa na wepesi wa kuonana na wahusika wakuu na kuweza kupata misaada haraka- TDC G Fast Track
  3. Utaweza kupata habari za nafasi za kazi Tanzania na hata ubalozini ( local staff) kwenye nchi unazoishi.
  4. Kila mwanachama anapotafuta mwekezaji na kumpitishia TDC G yeye ndio anakuwa mnufaika wa kwanza kimaslahi ya aina yoyote.
  5. BIMA ambayo itaweza kusaidia ndugu zako na hata wewe binafsi ukifariki mwili wako utaweza kupelekwa Tanzania (Inaandaliwa)
  6. Kusoma habari zote muhimu zilizo ndani ya web ya TDC G na pia kuwaona wanachama wote waliojiunga.
  7. Utawekwa kwenye magrupu yaTDC G na kupata habari za haraka, nyeti na muhimu
  8. Utaweza kupiga kura kwenye mikutano mikuu ya mwaka na kuweza kuchaguwa viongozi unaowataka .
  9. Kwenye makongamano ya TDC G unakuwa unapata unafuu wa bei (wakati wote tunaangalia maslahi ya wanachama wetu).
  10. Pata habari mapema(kipaumbele zaidi) kwa email au SMS
  11. Undugu dunia nzima kwa wanadiaspora