[vc_row][vc_column][vc_btn title=”CHANGI RAMBIRAMBI” color=”danger” align=”center” i_align=”right” i_icon_fontawesome=”fa fa-heart” add_icon=”true” link=”url:https%3A%2F%2Ftdcglobal.org%2Fsupport%2Frambirambi%2F||target:%20_blank|”][vc_column_text]Ndugu wanajumuiya ya TDC-Global,
Siku chache zilizopita, lilitokea tukio la kuhuzunisha. Palitokea mauaji ya kikatili jijini Dar-es-salaam, Tanzania ya kijana aitwaye Abdallah almaarufu kama Dullah. Dullah alikuwa mwanamuziki. Pamoja na wenzake wawili (majina yao), walikuwa wanaunda kundi la muziki linalojulikana kama The Mafik.

Habari za msiba wa Dullah zimegusa wengi. Sio tu kwamba amefariki akiwa katika umri mdogo sana, bali mauti yamemfika kupitia ukatili wa kutisha. Alikuwa kijana mdogo mwenye ndoto kemkem hususani kupitia kazi yake ya muziki.

Kwa TDC-Global, kifo cha Dullah ni pigo binafsi. Mnamo April mwaka huu wa 2019 kule Stockholm, Sweden na Estonia, Dullah na wenzake walishiriki nasi bega kwa bega katika kufanikisha uzinduzi rasmi wa TDC-Global. Dullah na wenzake sambamba na msanii Peter Msechu, walitoa burudani kwa siku zote mbili za kongamano. Walifanya vile kwa kujitolea. Hawakulipwa senti tano. Ni moyo wa kujitolea wa aina yake.

Kwa kuzingatia mchango wa Dullah kwa TDC-Global, tumeona si jambo la busara kuacha msiba wa Dullah kupita hivi hivi. Kwa kushirikiana nawe mwanajumuiya au wewe uliyeguswa na tukio hili, TDC-Global inakusanya michango ambayo itaiwakilisha kwa familia pamoja na kuchangia katika shughuli ya Siku Arobaini (40) ya marehemu.

Ili kukamilisha nia hii njema na ya kiungwana, tunaomba mchango wako wa hali na mali (na hususani kifedha). TDC-Global ina pokea Michango kwa kutumwa kwenda kwa Akaunti ya TDC Global kupitia

❤❤❤

Kwa taarifa au maelezo zaidi, unaweza kuwasiliana na TDC-Global kwa kupitia barua pepe info@tdcglobal.org.

Tunatanguliza shukrani za dhati. Mwenyezi Mungu akubariki na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

Norman Jasson
Mwenyekiti TDC Global.[/vc_column_text][vc_btn title=”CHANGI RAMBIRAMBI” color=”danger” align=”center” i_align=”right” i_icon_fontawesome=”fa fa-heart” add_icon=”true” link=”url:https%3A%2F%2Ftdcglobal.org%2Fsupport%2Frambirambi%2F||target:%20_blank|”][/vc_column][/vc_row]