wageni_lite
TDC Global

TDC Global

Taarifa Kuhusu Mkutano Mkuu 2021

Baraza la Diaspora Watanzania Duniani – TDC Global linayo furaha kubwa sana kuwatangazia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imeidhinisha Mkutano Mkuu wa TDC Global na siku ya Diaspora kufanyika jijini Dodoma Tanzania tarehe 23 – 26 June 2021.

Kutokana na maamuzi hayo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, TDC Global inawaomba wanachama na diaspora Watanzania duniani kujiandaa kushiriki katika fursa mbalimbali za Mkutano huo. Shime Diaspora tushirikiane
kuhudhuria tukio hili muhimu litakalofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania likiwa limeandaliwa na Diaspora wenyewe.

TDC Global inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden kwa ushirikiano na
msaada mkubwa unaotupatia TDC Global kwa masuala yote ya diaspora.

Maelezo zaidi na matangazo ya mkutano yataendelea kutolewa na viongozi wa
TDC Global kwa kadri yanavyokamilika.

TANGAZO LA MKUTANO MKUU 2021

Share this post