bana
mrina

mrina

UJUMBE KWA WATANZANIA DIASPORA

Wanadiaspora ni muhumu tukatambua kwamba ni  jambo la busara kwa sisi sote kuungana na kuwa na sauti moja kwa mafanikio ya wanadiaspora.

Na pia ni jukumu la kila mmoja wetu kuendelea kuwajulisha wanadiaspora kujiunga kwa pamoja katika umoja huu ulioanzishwa kwa ajili ya wanadiaspora kwa kupitia tivoti ya TDC Global  ( https://tdcglobal.org/member-register/ ).

(Tanzania Global Diaspora Council – TDC GLOBAL).

TDC Global ni umoja ambao unawakusanya watanzania diaspora popote walipo duniani kwa kupitia vyama vilivyopo katika nchi,majimbo na vitongoji wanamo ishi na pia kupitia mtu mmoja mmoja .Lengo na dhumuni ni kuwa na sauti moja.

Kila mwanadiaspora anatambua ya kwamba unapobadili uraia wa Tanzania unakuwa umepoteza haki zako zote za kumiliki ardhi na mengineyo ndani  ya nchi yako kwa mujibu wa sheria iliyopo.Na ili uweze kumiliki yakupasa upite kwa sheria za umiliki kama mgeni na si mtanzania.

Haya pia yanamkuta  mtanzania ambaye hajabadili uraia lakini ana watoto ambao wanauraia wa nje,nao pia watakuwa hawana sifa ya kumiliki mali,ardhi au kuridhi mali  kutoka kwa wazazi wao iwapo watakuwa na uraia wa nje.

Vilevile kuna wanadiaspora ambao walibadili uraia kwa njia za kujitafutia maisha kwa kusaidia familia zao nyumbani na wao binafsi na kujipatia uraia kwa kupitia nchi zingine Kwa njia moja au nyingine nao wanakumbwa na tatizo la kukosa umiliki kwa familia zao iwapo watakuwa na uraia wa nje.Hawa ni wazawa halisi.

Kuna wanadiaspora wanafunzi ambao walitoka nje ya nchi kimasomo na baadae kupata kazi na kuendelea na maisha ila wana uraia wa Tanzania,hawa pindi wapatapo watoto maswala ya watoto kutomiliki au kuridhi yatawakuta iwapo watoto wataamua kuchukua uraia wa nchi wanapoishi kutokana na hali halisi ya kimaisha au kimasomo.

Kwa haya machache wanadiaspora kwa ujumla ni muhimu kuweka tofauti zetu pembeni na kujiunga na umoja huu wa TDC GLOBAL tuwe na sauti moja na kuweza kuishawishi serikali ya awamu ya tano kutufikiria katika muono chanya na kuweza kutupokea katika kusaidiana kukuza uchumi wa nchi yetu kwa kututambua rasmi kwa kutupa (HADHI MAALUMU) ili nasi tuweze kuendelea kuufurahia uzawa wetu kwa kuweza  kuchangia uchumi wanchi yetu kwa vitendo kwa kupitia umoja wetu TDC GLOBAL,kwani wataona nini tunakifanya kwa pamoja.

Wanadiaspora tunawaomba mtembelee website ya TDC GLOBAL ili kuweza kusoma KATIBA na mengineyo.( https://tdcglobal.org) .

Kwa wale wenye maoni na usahuri wa kuboresha umoja wa TDC Glogal tuma maoni yako kwa njia ya email (maoni@tdcglobal.org) .

Nawatakieni kazi njema

 

Norman Jasson

NORMAN JASSON

Mwenyekiti TDC Global.

Share this post

Share on facebook
Share on google
Share on twitter
Share on linkedin
Share on pinterest
Share on print
Share on email