TDC Global
TDC Global

TDC Global

Utaratibu Wa Kupata “Password” TdcGlobal

TDC Global inapenda kuwajulisha wanachama na diaspora kwa ujumla utaratibu wa kupata nywila “password” mpya pale kutakapokuwa na uhitaji, kutokana na kusahau au kukosea nywila yako mara nyingi katika kuingia kwenye profile yako ya TDC Global.

Utaratibu wa sasa ni kama ifuatavyo:
1. Kumbuka barua pepe au jina unalotumia kuingia katika mtandao wa TDC Global- (Profile)
2. Tuma ujumbe kwa barua pepe admin@tdcglobal.org Andika ”ninaomba password mpya. Barua pepe yangu niliyojisajilia TDC Global ni ………….. (andika barua pepe yakoni muhimu katika kuwawezesha IT kufanikisha kukupatia nywila mpya)”.
3. Watendaji wa Tehama watabadilisha Nywila (Password) yako na kukutumia mpya katika barua pepe yako.
4. Ingia kwenye profile yako kwa kutumia password mpya na badilisha uliyotumiwa na uweke itakoyokuwa rahisi kwako kuikumbuka.
5. Endapo utakutana na tatizo lolote tuma ujumbe ”naomba msaada kupatiwa nywila mpya” kwenda WhatsApp namba 46724511963 au +358443101041.

Utaratibu huu ni wa muda wakati TDC Global kitengo cha Tehama kikiendelea kuboresha mtandao wetu ili kupata utaratibu mzuri wa kudumu.

Uongozi wa TDC Global unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea.

Diaspora na Nyumbani

TAARIFA KWA DIASPORA

 

Share this post