TDC Global
TDC Global

TDC Global

Uwekezaji Wa Biashara Tanzania – Diaspora

Salaam wana Diaspora wote popote mlipo.
Mlezi wa TDC Global Mhe Dkt. Willibrod P. Slaa anachukua fursa hii kuwakaribisha kwenye fursa nyingi za uwekezaji na biashara nchini Tanzania, wakati tunasubiri sera na sheria za Diaspora zikiandaliwa na serikali. Aidha serikali ya awamu ya sita ipo kwenye hatua nzuri ya kuboresha mazingira ya biashara kwa kufanyia marekebisho hata kabla ya sera rasmi ya Diaspora (ndani ya sera ya Mambo ya Nje) kukamilika. Marekebisho hayo ya sheria mbalimbali yanategemewa kuingia bungeni wakati wowote ikiwa ni pamoja na bunge la Septemba 2021.

Ni imani yangu wana Diaspora tutachukua fursa hiyo. Hata hivyo wako wana Diaspora, ambao tayari hata kwa sheria zilizopo tayari wameanza na wanawekeza Tanzania. Mfano wa hivi karibuni ni Kodak Eye Wear ambao Tarehe 30 July 2021 wanazindua kliniki ya kisasa ya macho na meno, jijini Dar Es Salaam, na kliniki zingine 2 mikoani, Tanzania. Tukiwa na nia moja
inawezekana. Hiyo ni fursa kwa wana Diaspora wenyewe kuwekeza. 

Kwa taarifa kamili, tafadhali soma nakala ambata hapa chini.

Share this post