• Mrina
  • August 22, 2018
  • Public
  • Mrina
  • July 29, 2018
  • Public
       

KATIBA YA TDC-GLOBAL

Ili kujenga jumuiya yenye nguvu, mshikamano, usawa umoja na amani, ni muhimu kuwa na msingi imara wa taratibu, kanuni na sheria za kutusimamia. TDC Global inaendeshwa chini ya katiba yake ambayo imechangiwa mawazo yake na kila diaspora wa kitanzani.

Katika kuhakikisha kuwa kila sauti ya mwana diaspora inasikika na kuhusika katika hatua hii muhimu, TDC Global inakuomba ushiriki katika mkakati wa kuboresha, kuijenga na kuipa nguvu katiba yetu.

Tafadhali, chukua muda wako wenye thamani, kujaza fomu ya mapendekezo na maboresho ya katiba ya TDC Global kwa kubofya kitufe hapo chini.