Baraza la diaspora Watanzania duniani – TDC Global linapenda kuwajulisha wanachama, diaspora na
umma kuwa, mkutano mkuu na kongamano la TDC Global 2024 vitafanyika tarehe 17, 18 na 19 Mei
2024, mjini Stockholm, Sweden. Mkutano unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa ndani ya meli ya Tallink Siljaline (Syphony)

TDC Global inawaomba watakao fikiwa na taarifa hii kuwajulisha diaspora, wadau wengine na
mashirika yanayoweza kushiriki katika mkutano mkuu na kongamano hilo kwa nia ya kulifanikisha.

Kwa taarifa zaidi za awali unaweza kuwasiliana na Dkt. Dickson Manga, naibu katibu mkuu, simu
+46704956650 au kuomba taarifa hitajika kwa kutumia barua pepe: mkutano@tdcglobal.org