MKUTANO MKUU NA KONGAMANO TDCG 2024
TDC Global inapenda kutoa taarifa muhimu kwa wanachama na washiriki wa mkutano mkuu na kongamano la mwaka 2024, litakalofanyika Stockholm Sweden na Helsinki Finland, kuanzia tarehe 17 hadi 19 Mei 2024 ili kurahisisha ushiriki wao kwa utulivu.
- Anwani ya bandarini – eneo la tukio ni: Hamnpirsvägen 10. 11574 Stockholm, Sweden
- Kutoka Airport hadi bandarini kwa gari binafsi (Tax) muda ni dakika 45.
Kwa usafiri wa umma tunashauri uwe na masaa mawili (2). - Kwa wanaotarajia kufika siku ya tukio tarehe 19 April 2024, tunawashauri
wachukue ndege zinazofika Stockholm Arlanda Airport saa nne asubuhi
(10:00) ili kufika eneo la tukio kwa utulivu - Kwa watakao kuja mapema na kuhitaji hoteli, tunawashauri kutafuta hoteli
karibu na bandarini (seach hotel near Terminalen Stadsgarden 116 30
Stockholm)
Tarehe Muda | Tukio | Mahali |
---|---|---|
19 April 2024 14:00 | Tutaanza kuingia melini. | |
19 April 2024 15:00 | Mkutano mkuu TDC Global utaanza katika ukumbi wa mikutano ndani ya meli ya Cinderella Vikingline | Melini |
19 April 2024 16:30 | Meli itaondoka bandarini Stockholm. Tunashauri uwepo bandarini kabla ya saa nane mchana (14:00), ili kuweza kusaidiwa na watendaji wa TDC Global katika mapokezi. | |
19 April 2024 18:00 | Mkutano mkuu TDC Global 2024 utafungwa. | |
19 April 2024 19:30 | Chakula cha usiku cha pamoja. | |
20 April 2024 07:00 | Kifungua kinywa (Breakfast) | |
20 April 2024 10:00 | Kufika Helsinki Finland | |
20 April 2024 12:00 – 17:30 | kongamano la ECO tourism litaanza ndani ukumbi wa mikutano wa meli. | |
20 April 2024 17:15 | Meli itaanza safari ya kurudi Stockholm Sweden | |
21 April 2024 10:00 | meli itafika bandari ya Terminalen Stadsgården, 116 30 Stockholm. | |
Tunashauri wanaotarajia kuondoka na ndege tarehe 21 April 2024 kurudi makwao, kuchukua ndege zinazo ondoka Sweden kuanzia saa nane mchana (14:00) ili kusafiri hadi airport kwa utulivu.
Muda wa kujisajili kwenye mkutano umeongezwa hadi tarehe 21 March JIANDIKISHE SASA
Kushiriki katika mkutano jaza fomu na lipia ushiriki kupitia kiunganishi hiki: https://tdcglobal.org/mkutano-mkuu
Kwa msaada wa haraka siku ya tukio tumia simu namba +46704470323. Taarifa zaidi za mkutano zitaendelea kutolewa kwa kadri zinavyokamilika.
Tunatanguliza shukrani kwa ushirikiano mnaotupatia.