Mkutano Mkuu

Baraza la diaspora Watanzania duniani – TDC Global linapenda kuwakaribisha kushiriki kwenye mkutano mkuu na kongamano la diaspora 2025. Mkutano na kongamano hilo vitafanyika katika hotel ya Grand Excelsior iliyopo Deira, Dubai, UAE kuanzia tarehe 25 hadi 27 April 2025.

Washiriki wote wanatakiwa kukamilisha usajili wao kabla ya tarehe 1 Januari 2025. Kujisajili tumia kiunganishi hiki:
https://tdcglobal.org/tdc-global-2025-agm-dubai-registration/.

JIANDIKISHE HAPA

Unaweza pia kutumiwa kiunganishi hicho cha kujisajili kwa WhatsApp au barua pepe yako kwa kutuma ujumbe huu ”Nitumie taarifa za kujisajili katika mkutano, Dubai 2025” kwenda namba +971552835590.

Pamoja na mkutano mkuu na uchaguzi wa viongozi, kongamano litatumika kutangaza fursa za uwekezaji na utalii unaojali mazingira nchini Tanzania. Washiriki watapata pia fursa ya kutangaza shughuli zao, kutembelea jiji la Dubai usiku, na safari ya boti itakayo jumuisha chakula cha pamoja.

Kwa msaada wa kukamilisha ushiriki wako kitaasisi au kibinafsi, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe mkutano@tdcglobal.org. TDC Global inawakaribisha diaspora na nyumbani

kushiriki katika mkutano huu wenye fursa nyingi za kimaendeleo na uwekezaji.

Upatapo taarifa hii tafadhali wajulishe na wengine.