MKUTANO MKUU NA KONGAMANO TDCG 2024

TDC Global inapenda kutoa taarifa muhimu kwa wanachama na washiriki wa mkutano mkuu na kongamano la mwaka 2024, litakalofanyika Stockholm Sweden na Helsinki Finland, kuanzia tarehe 17 hadi 19 Mei 2024 ili kurahisisha ushiriki wao kwa utulivu.

 1. Anwani ya bandarini – eneo la tukio ni: Hamnpirsvägen 10. 11574 Stockholm, Sweden
 2. Kutoka Airport hadi bandarini kwa gari binafsi (Tax) muda ni dakika 45.
  Kwa usafiri wa umma tunashauri uwe na masaa mawili (2).
 3. Kwa wanaotarajia kufika siku ya tukio tarehe 19 April 2024, tunawashauri
  wachukue ndege zinazofika Stockholm Arlanda Airport saa nne asubuhi
  (10:00) ili kufika eneo la tukio kwa utulivu
 4. Kwa watakao kuja mapema na kuhitaji hoteli, tunawashauri kutafuta hoteli
  karibu na bandarini (seach hotel near Terminalen Stadsgarden 116 30
  Stockholm
  )
Tarehe MudaTukioMahali
19 April 2024 14:00Tutaanza kuingia melini.
19 April 2024 15:00Mkutano mkuu TDC Global
utaanza katika ukumbi wa mikutano ndani ya meli ya Cinderella Vikingline
Melini
19 April 2024 16:30Meli itaondoka bandarini Stockholm. Tunashauri uwepo bandarini kabla ya saa nane mchana (14:00), ili kuweza kusaidiwa na watendaji wa TDC Global katika mapokezi.
19 April 2024 18:00Mkutano mkuu TDC Global 2024 utafungwa.
19 April 2024 19:30Chakula cha usiku cha pamoja.
20 April 2024 07:00Kifungua kinywa (Breakfast)
20 April 2024 10:00Kufika Helsinki Finland
20 April 2024 12:00 – 17:30kongamano la ECO tourism litaanza ndani ukumbi wa mikutano wa meli.
20 April 2024 17:15 Meli itaanza safari ya kurudi Stockholm Sweden
21 April 2024 10:00 meli itafika bandari ya Terminalen Stadsgården, 116 30 Stockholm.
Matukio kwa muhtasari

Tunashauri wanaotarajia kuondoka na ndege tarehe 21 April 2024 kurudi makwao, kuchukua ndege zinazo ondoka Sweden kuanzia saa nane mchana (14:00) ili kusafiri hadi airport kwa utulivu.

Muda wa kujisajili kwenye mkutano umeongezwa hadi tarehe 21 March JIANDIKISHE SASA

Kushiriki katika mkutano jaza fomu na lipia ushiriki kupitia kiunganishi hiki: https://tdcglobal.org/mkutano-mkuu

Kwa msaada wa haraka siku ya tukio tumia simu namba +46704470323. Taarifa zaidi za mkutano zitaendelea kutolewa kwa kadri zinavyokamilika.

Tunatanguliza shukrani kwa ushirikiano mnaotupatia.