Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden umepokea barua kutoka kampuni ya Nala Inc ikiomba kutambulishwa kwa watanzania na Jumuiya zake waishi katika nchi za uwakilishi. Kampuni ya NALA Inc inamilikiwa na diaspora Mtanzania anaeitwa Bw. Benjamin Fernandes. Kampuni hii inatoa hduma za kutuma na kupokea fedha kupitia Benki na mitando ya Simu za mkononi nchini Tanzania. Aidha kampuni hiyo huto huduma ya kutuma fedha katika nchi Ishirini na moja (21) Ulimwenguni. Nchi hizo ni Austria, Cyprus, Estonia, Finland, Hispania, Ireland, Italia, Latvia, Lithuania, Luxembour, Malta, Marekani, Slovakia, Slovenia, Ubelgiji, Ufaransa, Ugiriki, Uingereza, Uholanzi na Ureno.
Kwa Afrika kmapuni ya NALA Ink inatoa huduma ya kutuma na kupokea fedha nchini Tanzania, Rwanda, Kenya, Uganda, Senegal, Ghana na Nigeria. Hivyo Ubalozi unapenda kuwajulisha Viongozi wote kuhusu Kampuni hii, ili kuweza kufikisha taarifa za kampuni hii kwa diaspora wote waliopo katika maeneo yenu.
Barua rasmi, imeambatanishwa hapa chini.