Baraza la diaspora Watanzania duniani-TDC Global, linapenda kuwajulisha wanachama na diaspora Watanzania duniani kuwa mkutano mkuu na uchaguzi wa viongozi uliofanyika tarehe 11 na 12 Julai 2023 Dar es Salaam, Tanzania ulimalizika salama na ulifikia malengo yake.
Yatokanayo na mkutano na uchaguzi huo ni kupatikana kwa viongozi wa juu wa TDC Global-Kamati Kuu, watakao iongoza taasisi kwa muda wa miaka miwili. Kuanza kwa kipindi hicho kipya cha uongozi kunapelekea kumalizika kwa muda wa uongozi kwa viongozi wengine wa taasisi kwa mujibu wa katiba kifungu namba 13-F. Hivyo basi TDC Global inawajulisha wanachama wenye nia ya kushiriki katika kuijenga taasisi wakiwa viongozi wa kamati, kuwasilisha majina yao kwa uongozi kabla ya tarehe 18 Augusti 2023 saa sita usiku saa za Tanzania kwa uchaguzi utakaofanywa na kamati kuu.
Kwa watakao omba kuchaguliwa kuongoza kamati za TDC Global, tafadhali wazingatie katiba ya TDC Global kifungu namba 13-A. Nafasi zinazo hitaji kuombwa ni hizi zifuatazo:
Nafasi za uongozi kwa kila kamati:
Wanachama wanaweza kujaza fomu za kuomba kuchaguliwa katika nafasi za mwenyekiti, katibu au ujumbe, wa kamati wanayokusudia kuitumikia. Uchaguzi wa viongozi utafanywa na kamati kuu ya TDC Global baada ya tarehe 18 August 2023.
Kujaza fomu na kuiwasilisha, tafadhali bonyeza kiungo hapa chini.