cropped-tdc-globsl-logo-removebg-preview.pngcropped-tdc-globsl-logo-removebg-preview.pngcropped-tdc-globsl-logo-removebg-preview.pngcropped-tdc-globsl-logo-removebg-preview.png
  • Home
  • About Us
    • About TDC
      • Wazee
      • Wanawake
    • Katiba
    • Organisation Chart
    • Partners
      • Tanzanian Embassy in Sweden
      • Ministry of Home Affairs
      • Ministry of Foreign Affairs and EA Relations
      • Swedish Embassy in Tanzania
      • Tanzania Investment Center
      • Tanzania Banks
        • Equity Bank
        • Azania Bank
        • CRDB Bank
  • Membership
    • Register
    • Subscription Plan
  • Media & Resources
    • Video Gallery
    • Photo Gallery
    • News & Events
  • Contact Us
  • Login
✕
UCHAGUZI WA KAMATI 2023
9 August 2023

Baraza la diaspora Watanzania duniani-TDC Global, linapenda kuwajulisha wanachama na diaspora Watanzania duniani kuwa mkutano mkuu na uchaguzi wa viongozi uliofanyika tarehe 11 na 12 Julai 2023 Dar es Salaam, Tanzania ulimalizika salama na ulifikia malengo yake.

Yatokanayo na mkutano na uchaguzi huo ni kupatikana kwa viongozi wa juu wa TDC Global-Kamati Kuu, watakao iongoza taasisi kwa muda wa miaka miwili. Kuanza kwa kipindi hicho kipya cha uongozi kunapelekea kumalizika kwa muda wa uongozi kwa viongozi wengine wa taasisi kwa mujibu wa katiba kifungu namba 13-F. Hivyo basi TDC Global inawajulisha wanachama wenye nia ya kushiriki katika kuijenga taasisi wakiwa viongozi wa kamati, kuwasilisha majina yao kwa uongozi kabla ya tarehe 18 Augusti 2023 saa sita usiku saa za Tanzania kwa uchaguzi utakaofanywa na kamati kuu.

Kwa watakao omba kuchaguliwa kuongoza kamati za TDC Global, tafadhali wazingatie katiba ya TDC Global kifungu namba 13-A.  Nafasi zinazo hitaji kuombwa ni hizi zifuatazo:

  1. Kamati ya Mahusiano kwa Umma. (Public Relations Committee)   
  1. Kamati ya Tehama na Mitandao ya Kijamii. (IT and Social Media Committee)
  1. Kamati ya Biashara na Uchumi (TDCGCC - Chamber of Commerce Committee)
  1. Kamati ya Masuala ya Wazee (Elderly Affairs Committe)
  1. Kamati ya Vijana (Youth Affairs Committee)
  1. Kamati ya Wanawake (Women Affairs Committee)
  1. Kamati ya Ustawi wa Jamii ( Social Welfare Committee)
  1. Kamati ya Taaluma, Uvumbuzi na Ujuzi (Professionals, Skills and Innovation Committee)
  1. Kamati ya Kutunisha Mfuko (Philandthropy and Fundraising Committee)
  1. Kamati ya Sanaa, Utamaduni na Michezo (Arts, Culture and Sports Committee)

Nafasi za uongozi kwa kila kamati:     

  1. Mwenyekiti  wa kamati
  2. Katibu wa kamati
  3. Ujumbe wa kamati - nafasi tano

Wanachama wanaweza kujaza fomu za kuomba kuchaguliwa katika nafasi za mwenyekiti, katibu au ujumbe, wa kamati wanayokusudia kuitumikia. Uchaguzi wa viongozi utafanywa na kamati kuu ya TDC Global baada ya tarehe 18 August 2023.

Kujaza fomu na kuiwasilisha, tafadhali bonyeza kiungo hapa chini.

Fomu Nafasi Za Uongozi Wa Kamati
Share
0

Related posts

9 August 2023

Taarifa Uchaguzi Wa Kamati


Read more
9 August 2023

UCHAGUZI WA KAMATI 2023


Read more
4 May 2023

Mkutano Mkuu TDC Global 2023


Read more

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Diaspora na Nyumbani
Pamoja Tunaweza

Connect with TDC Global
Useful link
  • Home
  • Contacts
  • Login
Consultant

TDC Global
+46765643948

info@tdcglobal.org

© 2023 TDC Global | All Rights Reserved

Register Now